Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango amewataka viongozi na maafisa wa magereza kubadili mtazamo, ili kuendana mazingira ya sasa kwa kuwa mfumo na Sheria za magereza zimerithiwa kutoka kwa wakoloni.
Makamu wa Rais Dk.Mpango ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza uliofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Msalato, Dodoma.
Makamu wa Rais pia ameitaka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuharakisha mchakato wa marekebisho ya Sheria kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai na hali ya sasa.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Msauni, amesema Wizara itaendelea kusimamia marekebisho na maboresho ya Jeshi la Magereza ikiwa ni pamoja na kutenganisha majukumu ya urekebu ya Jeshi la hilo, na majukumu ya kibiashara kufanywa na shirika la uzalishaji mali (SHIMA).