Back to top

FIFA YATUPIWA LAWAMA KWA KUTOIFUNGIA ISRAEL

22 March 2024
Share

Wachezaji wa soka wa Palestina, viongozi na mashabiki wamelitupia lawama Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), kwa kushindwa kuiwekea vikwazo pamoja na kuipiga marufuku Israel, kutokana na kuendelea kwa vita dhidi ya Gaza, ambapo zaidi ya watu 31,000 wakiwemo watoto 13,000 wameuawa.
.
Lawama hizo kwa FIFA, zimeongezeka katika miezi ya hivi karibuni, huku ikilinganishwa na msimamo wa Shirikisho hilo wa kuifungia Urusi ambayo ilikuwa mgombea mwenye nguvu katika mchujo wa kuwania Kombe la Dunia la FIFA la Qatar 2022, pamoja na vilabu vya soka vya nchi hiyo, kushiriki katika shughuli zote za soka za kimataifa wakati Urusi ilipovamia Ukraine, uamuzi ambao uliidhinishwa na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo.
.
Hata hivyo, takribani miezi sita ya vita huko Gaza, FIFA imekaa kimya, huku Israel ikijiandaa kucheza na Iceland katika michuano ya kufuzu Euro 2024.