
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeondoa hofu wananchi kuhusiana na uwepo wa mayai feki nchini, baada ya kutokea taharuki mtandaoni kufuatia video iliyosambaa ikionyesha kiwanda kinachotengeneza mayai.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Hezron Nonga, ambapo amesema wizara hiyo inafuatilia kwa kina aliyesambaza taarifa ya kiwanda cha kutengeneza mayai katika kata ya Goba Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam achukuliwe hatua kali.
Amesema "Wizara inapenda kuwatoa hofu wananchi kuwa imefuatilia suala hilo kwa kina na kujiridhisha kuwa tarifa hizo sio za kweli, ni upotoshaji na hivyo kuitaka jamii kuipuuza'Amemesema Nonga.
"Oktoba 12 mwaka huu kumekuwa na picha ya mayai mengi na taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uwepo wa kiwanda cha kutengeneza mayai katika Kata ya Goba, Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es Salaam"