Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekubaliana na hoja za utetezi kuhusu pingamizi la kutopatiwa dhamana, lililokuwa limewekwa na Jamhuri/ serikali dhidi ya aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni na baadaye Ubungo, Dar es Salaam Boniface Jacob (Boni Yai), hivyo Boniface amepatiwa dhamana inayoendana na masharti yatakayowekwa kwenye shauri la msingi, ambalo sasa linaendelea.
Maamuzi hayo madogo ndani ya kesi ya msingi yametangazwa Mahakamani hapo na Hakimu mkazi Mkuu Franco Kiswaga wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, ambapo shauri hilo lililetwa Mahakamani hapo kwa ajili ya kusomwa hukumu ya kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.
Jacob, maarufu kama Boni Yai, alikuwa akikabiliwa na kesi ya uchapishaji taarifa za uwongo kwenye mitandao.