Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro inakabiliwa na uhaba mkubwa wa mitungi ya Oksijeni kutokana ongezeko la wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa upumuaji ambapo mgonjwa mmoja hulazimika kutumia mitungu 10 hadi 12 kwa siku.
Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Prof.Gilliard Masenga amesema hospitali hiyo kwa siku hutumia mitungi 400 ya Oksijeni ambayo bado haitoshelezi, ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa wenye mahitaji ya Oksijeni.
Amesema suala la kuchukua hadhari ni lazima ikiwa ni pamoja na kufuata tahadhari zinazotolewa na wataalam wa afya kula vyakula vyenye virutubisho ili kuongeza kinga mwilini.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw.Stephen Kagaigai ametoa maagizo kwa jeshila polisi kuhakikisha wanazuia mikusanyiko yote isiyokuwa ya ulazima pamoja pamoja na kuwataka wananchi kuchukua hadhari za kujikinga na Corona.