Back to top

JAKAYA KIKWETE FEKI APANDISHWA MAHAKAMANI

24 September 2024
Share

 Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imempandisha kizimani mkazi wa Mabwe pande, Shembiu Shekilaghe(38) akikabiliwa na mashtaka ya kutoa taarifa za uongo na kujiwasilisha kama yeye ni Jakaya Mrisho Kikwete huku akijua sio kweli. 

Wakili wa Serikali, Salma Jafari alidai hayo hapo jana tarehe 23 Septemba, 2024 alipokuwa akimsomea mshtakiwa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hawa Magesa mshtakiwa alipofikishwa mahakamani hapo. 

Jafari alidai mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka 14, huku mashitaka ya kwanza ya pili na tatu  yakiwa ni kutoa taarifa za uongo.


Ilidaiwa Septemba 2,2024 mshtakiwa akiwa katika eneo lisilojulikana ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa taarifa za uongo kupitia Akaunti ya mtandao wa kijamii ya Facebook yenye jila la Mrisho Jakaya Kikwete akisema;


“Ukiweka akiba ya 49,000 utapata mkopo wa laki tatu marejesho ni Sh 30,000 kila mwezi kwa muda wa miezi 10,”