Back to top

Jeshi la uhamiaji Mwanza lakamata wahamiaji haramu 24 kanisani.

08 October 2020
Share

Jeshi la uhamiaji mkoa wa Mwanza limewakamata wahamiaji haramu 24 kutoka nchi za Burundi na Rwanda kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria na taratibu waliokutwa wakifanya kazi katika kanisa la Baba Godi lililopo eneo la Kangae ‘A’ wilaya ya Ilemela jijini Mwanza pamoja na viongozi saba wa kanisa hilo ambao ni raia wa Tanzania wanaotarajiwa kufikishwa mahakamani.

Akizungumza na vyombo vya habari Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Bahati Mwaifuge amesema Jeshi la uhamiaji kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi walifika katika kanisa hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema na kufanikiwa kuwakamata watu hao.