Back to top

Jozi za viatu vya ngozi milioni 50 huagizwa nchi za nje kila mwaka.

16 August 2020
Share


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Mpina amesema serikali inalazimika kuagiza jozi za viatu vya ngozi milioni 50 nje ya nchi kila mwaka kutokana na viwanda 20 vilivyopo hapa nchini kushindwa kuzalisha bidhaa zinazokidhi soko la ndani. 

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi kilimanjaro, Waziri Mpina amesema kwa mwaka viwanda vyote huzalisha jozi milioni 1.2 ambazo hazitoshelezi mahitaji ya soko la ndani.

Amesema kwa sasa kuna haja kwa Tanzania kuhakikisha wanatumia ngozi zinazozalishwa hapa nchini kwa kuongeza thamani bidhaa za ngozi ili kuzalisha bidha zenye ubora zitakazokidhi ushindani wa masoko ya ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Afisa wa Dawati la Sekta Binafsi Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Augustino Mshanga amesema kwa sasa Tanzania inazalisha bidhaa za ngozi chini ya viwango kwa asilimia 20.

Naye mkuu wa idara ya fedha katika kiwanda cha bidhaa za ngozi kilimanjaro Bw.Shalua Magandi amesema kiwanda hicho ambacho kinatajaia kuanza uzalishaji rasmi hivi kitakuwa na uwezo wa kuzalisha jozi za viatu zaidi milioni 1.2 kwa mwaka.