
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amezitaka kampuni kubwa za meli duniani kuwekeza Tanzania baada ya marekebisho ya demokrasi ya kiuchumi kufanywa katika sekta muhimu za ukuzaji wa uchumi ikiwemo sekta ya ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano.
Prof.Kabudi ametoa kauli hiyo katika kikao kazi kati ya serikali na wamiliki wa meli kubwa duniani kilichofanyika katika jengo la mamlaka ya bandari (TPA) huku akizungumzia lengo haswa la serikali la kufanya maboresho katika bandari zake nchini.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe ndiye aliyeongoza kikao hicho ambapo amesema matokeo chanya ya maboresho ya gati la bandari yameanza kuonekana mara baada ya meli kubwa iliyobeba shehena ya mbolea kuwasili.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari nchini Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema malaka hiyo inachotaka kufanya ni kuhakikisha inatengeneza mtandao mzuri wa ufanyaji wa kazi kwenye bandari zote nchini.