Kipande cha keki cha miaka 77 kilichokatwa kwenye keki ya harusi ya Malkia Elizabeth II na Prince Philip, kimeuzwa kwa £2,200 ($2,800) wiki hii.
Keki hiyo, ambayo haifai kuliwa tena, ilidumu kwa karibu miongo minane tangu siku ya harusi ya Elizabeth II na Philip mnamo Novemba 20, 1947.
Bado keki hiyo imefungwa vizuri kwenye kisanduku kidogo chenye nembo ya fedha, cha Binti Elizabeth wa wakati huo.
Sanduku lililohifadhia keki hiyo, lilitumwa kutoka Buckingham Palace kwenda kwa Marion Polson, mlinzi wa nyumba katika Holyrood House huko Edinburgh, Scotland, kama zawadi kutoka kwa wanandoa hao wa kifalme.
Kando ya keki hiyo, Polson alipokea barua kutoka kwa Elizabeth ikimshukuru kwa zawadi hiyo.