
Kikosi cha Doria ya kupambana na uvuvi haramu Ziwa Victoria kanda ya Ukerewe mkoani Mwanza, kuanzia Agosti 3 wiki ijayo kitaanza kutumia Mahakama inayotembea kutoa hukumu ya kifungo cha miezi sita hadi mwaka mmoja kwa watu wanaoendelea kujihusisha na uvuvi haramu wa kutumia makokoro na nyavu za timba.
Kamanda wa Operesheni maalum ya kuzuia uvuvi haramu mwaka 2018 Ziwa Victoria kanda ya Ukerewe Didas Mtambalike ametoa angalizo hilo wakati akizungumza na wavuvi wa kambi ya Bukimwi kata ya Ngoma wilayani humo.
Kilo 400 za samaki waliovuliwa kwa kutumia zana haramu zilizokamatwa katika operesheni hiyo zimegawiwa kwa wanafunzi wa chuo cha ualimu Murutunguru wilayani Ukerewe.