
Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limetangaza aina mpya ya kirusi cha Corona, kilichogundulika hivi karibuni nchini Afrika Kusini kuwa ni chenye kutia wasiwasi na kukiita jina la Omicron. Aina hii mpya ya kirusi cha Corona iliripotiwa kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini mnamo Novemba 24, huku ikibainika kuwa tayari imeenea katika mataifa ya Botswana, Ubelgiji, Hong Kong na Israeli.