Back to top

Lukuvi atoa siku tatu kwa maafisa ardhi halmashauri ya Monduli.

10 September 2018
Share

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Lukuvi ametoa muda wa siku tatu kwa watalamu wa ardhi katika halmashauri za Arusha na Monduli kuwasilisha hati za shamba lenye mgogoro na kibali cha kusafisha shamba hilo kilichotolewa kwa kampuni ya Tanfoam.

Hatua hiyo ya Waziri Lukuvi anaifikia baada ya kutembelea shamba hilo lenye ukubwa wa zaidi ya ekari elfu tatu katika kijiji cha Lengilaroti ambalo halijaendelezwa kwa zaidi ya miaka thelathini sasa.

Awali wakizungumza mbele ya Waziri wananchi wa kata tatu za Lokisale, Naalaram na Lemoti wanaopakana na shamba hilo wanasema licha ya shamba hilo kutokuendelezwa lakini wananchi wamekua wakipata manyanyaso kutoka kwa walinzi wa shamba ikiwa ni pamoja na kuuawa kwa mifugo.

Miongoni mwa maafisa wa ardhi waliopewa muda wa kuwasilisha hati hizo ni afisa ardhi mteule wa halmashauri ya Arusha na Monduli Rehema Jato ambaye katika mahojiano na Waziri Lukuvi anaeleza kuwa tayari walishatoa notisi kwa kampuni hiyo mwaka 2016.