![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/InShot_20211222_092344412.jpg?itok=B3Ywzqgp)
Mabasi tisa ya abiria katika stendi kuu ya mabasi ya Nyegezi jijini Mwanza yang'olewa namba na kuzuiwa kuendelea na safari baada ya kubainika kuwa ni mabovu kupitia ukaguzi ulioongozwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Wilbroad Mutafungwa.
Kamanda Mutafungwa amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na wamiliki wa magari kutotumia kipindi hiki cha msimu wa kuelekea sikukuu kinachokua na abiria wengi kuingiza magari mabovu barabarani ili wajipatie kipato.