
Majambazi watano waliokuwa wakirushiana risasi na askari polisi wilayani Korogwe mkoani Tanga wameuawa baada ya jaribio lao la kwenda kupora mishahara ya wafanyakazi wa mashamba ya mkonge ya kampuni ya Toronto iliyopo wilayani humo kushindikana.
Akizungumza katika eneo la tukio,kamanda wa polisi mkoani Tanga kamishna Msaidizi Edward Bukombe amesema katika majibizano hayo mmoja kati ya majambazi hayo yaliyokuwa na silaha aina ya shotgun yenye risasi tano na bastola moja alimpiga risasi kifuani Afisa upelelezi wa wilaya ya korogwe Samson Mwandambo lakini vazi la kuzuia risasi alilokuwa amevaa ndio lililomnusuru na kifo .
Kufuatia hatua hiyo Kamanda wa polisi mkoani Tanga amewahakikishia wananchi kuwa waendelee kutoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa wahalifu na jeshi la polisi litaendelea kuficha jina la mtu yeyote atakayelisaidia jeshi na kuwezesha kukamatwa wahalifu.