Back to top

Makontena ya Makonda yakosa wateja.

01 September 2018
Share

Mnada wa makontena 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda Bandarini umefanyika bila mafanikio baada ya wateja kutaja bei chini ya bei elekezi iliyotolewa kwenye mnada .

Mnada huo umefanyika eneo la Bandari kavu ya Malawi Cargo ukiendeshwa na kampuni ya udalaliya Yono Auction Mart ambapo wanunuzii wametakiwa kuwa na kitambulisho, leseni ya gari au pasipoti na kulipa angalao asilimia 25 ya bei siku ya mnada  ambapo vitu vilivyokuwa kwenye makontena hayo ni samani za ofisini kama viti meza na makabati.

Hii ni mara ya pili kwa mnada huo kufanyika baada ya Agosti 25 kushindwa ambapo makontena hayo yalianza kuuzwa na wateja kutaja bei ya chini.

Kotena moja linauzwa kwa milioni 60 ili kupata kiasi kilichokadiriwa cha bilioni 1.2 kwa makotena yote 20.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo Scholastica Kevela amesema wataendelea na mnada huo jumamosi ijayo.