Back to top

MAMA SAMIA LEGAL AID KUENDELEA KATIKA MIKOA 5

17 February 2025
Share

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, ametangaza kuendelea kwa Kampeni  ya  Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, maarufu kama Mama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC), katika Mikoa Mitano. 

Waziri Ndumbaro amesema hayo mkoani Ruvuma  alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari.

Amesema,  Kampeni hiyo  ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya  kutoa Msaada wa Msaada Kisheria, Elimu ya msingi juu ya masuala mbalimbali ya Kisheria, na kusaidia utatuzi wa Migogoro ya Wananchi katika ngazi mbalimbali za Jamii. 

“Hadi sasa, Kampeni hii imetekelezwa katika mikoa 17 na itaendelea katika Mikoa mingine mitano katika awamu hii ambapo Uzinduzi wake unatarajiwa kuanza Februari 18, 2025 katika  Mkoa wa Mwanza”. Amesema Ndumbaro 

Aidha,  tarehe 19 Februari 2025, Uzinduzi utafanyika katika Mkoa wa  Lindi na kuhudhuriwa na  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb).

Katika taarifa yake Waziri Ndumbaro amesema kuwa tarehe  Februari 24, 2025, Mikoa mitatu ya Mbeya, Rukwa na Pwani itazindua rasmi Kampeni ya Mama Samia Legal Aid.

Kwa mujibu wa Ndumbaro amesema ifikapo Machi 2025, Kampeni hii itakuwa imekamilika katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar, lengo kuu likiwa ni kuhakikisha kila Mwananchi anapata Haki ya Msaada wa Kisheria bila ubaguzi wowote. 

Kampeni ya Mama Samia Legal Aid inalenga kujenga jamii yenye Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi Chanya, na Taifa lenye  Amani.

Kupitia Kampeni hiyo mafunzo mbalimbali yanayotolewa ikiwa ni pamoja na  Utawala Bora na Sheria kwa ajili ya kujenga msingi thabiti wa Utawala wa Sheria Nchini.