Serikali imeanza kuchukua hatua kukabiliana na ugonjwa wa Utapiamlo kwa kufunga vifaa maalum vya kuongeza virutubisho vya Vitamin na madini kwenye mashine zote za kukoboa na kusaga nafaka hasa vijijini ambako wananchi hawana uelewa wa kutosha kuhusu maswala ya virutubisho na lishe bora.
Akizungumza na wadau wa afya ya lishe kutoka sekta binafsi na watendaji wa mamlaka mbalimbali zinazohusika na maswala ya vyakula na usindikaji,Afisa lishe wa Wizara ya afya na ustawi wa jamii kitengo cha uzalishaji elizabeth ndaba amesema hasi sasa mikoa ya songwe na Mbeya ina kiwango cha 38% ya udumavu zaidi ya kiwango cha kitaifa ambacho ni 34% hivyo bado serikali haijafanya vizuri kukabiliana na tatizo hilo,huku Dkt.Musa mwalemile akitaja sababu za kufunga vifaa vya virutubisho kwenye mashine za nafaka.
Bi.Chiku Gallawa mkuu wa mkoa wa Songwe amewataka maafisa afya wabadilike kifikra na kuwajibika kwa majukumu yao hasa kwa wananchi wa vijijini akidai kuwa kikao kilichowakutanisha na wadau wengine wa lishe kilete mabadiliko ya haraka iwezekanavyo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Katika kijiji cha Majengo kata ya Chiwezi nimezungumza na wananchi ambao bado wanaamini serikali ina dhamira njema kupambana na udumavu lakini swala la maafisa lishe kutofika vijijini ni changamoto nyingine.