Back to top

Mawasiliano ya barabara mikoa ya Mbeya, Tabora na Singida yakatika.

28 April 2020
Share

Mawasiliano ya barabara kati ya mikoa ya Mbeya, Tabora na Singida yamekatika baada ya mvua zinazoendelea kunyesha kusomba kingo za daraja la Mto Biti, lililopo Kata ya Mafyeko Wilayani Chunya.

Hali hiyo imesababisha magari kushindwa kupita na kuleta usumbufu mkubwa kwa wananchi na wasafiri wanaotumia barabara hiyo.

Abiria wanaosafiri kati ya mikoa hiyo wamekwama katika Kijiji cha Bitimanyanga, Kata ya Mafyeko Wilayani Chunya baada ya kingo za daraja la Mto Biti kusombwa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha.

Meneja wa Wakala wa Barabara nchini, mkoa wa Mbeya, Mhandisi Elizary Rweikiza ambaye amesema hatua zimeanza kuchukuliwa kurejesha mawasiliano katika eneo hilo.