Serikali ya mkoa wa Mtwara imesema mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Mtwara Evodi Mmanda yanafanyika Mtwara na yatasimamiwa na serikali na kuhudhuriwa na watu wasiozidi kumi lengo likiwa kusimamia taratibu za wizara ya afya kuzuia mikusanyiko katika kipindi hiki cha maambukizi ya virusi vya corona.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amesema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari huku akisisitiza kutokupuuza kufuata maelekezo ya wizara ya afya ya kijikinga na ugonjwa wa corona.