Back to top

MIGOMO YA MADEREVA MPAKANI KUTATULIWA

15 October 2022
Share

Tanzania na Zambia zimekubaliana kuimarisha mifumo ya utendaji kazi, ili kumaliza migomo ya madereva katika mpaka wa Tunduma - Nakonde unaozitenganisha nchi hizo mbili.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema makubaliano hayo yamefikiwa  katika mkutano wa kumi wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia katika Ngazi ya Mawaziri uliofanyika jijini Lusaka, Zambia.

Akifungua mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt.Stergomena Tax, amesisitiza dhamira ya wazi ya Serikali ya Tanzania katika kuendelea kuimarisha ushirikiano na serikali ya Zambia kwa kufanya maboresho na usimamizi wa karibu katika sekta za kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.

Ametaka nchi hizo zinatakiwa kuweka mazingira wezeshi kwa sekta za umma na binafsi ya kurahisisha shughuli za biashara na usafirishaji, ili kuinua uchumi wa nchi zote mbili.