Kikosi cha Ukaguzi cha Mamlaka ya Jaji safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Dodoma (DUWASA) kwa kushirikiana na Jeshi la polisi wamemkamata Mkurugenzi wa Chuo cha Mafunzo ya upishi cha Dati jijini Dodoma kakongwe misambano baada ya kubaini taasisi yake kujiunganishia maji kinyume na sheria na kusababisha hasara kwa mamlaka hiyo na serikali
Akizungumzia tukio hilo Mkaguzi wa mifumo ya maji kwa wateja wa DUWASA Alex Makelema anasema walianza kutilia mashaka chuo hicho baada ya kubaini matumizi kidogo ya maji ambayo hayalingani na mahitaji ya taasisi hiyo na kufuatilia ndipo walipobaini mifumo ya maji kuunganishwa kitaalamu bila kuwa na uwiano na mita inayosoma ankara.
Mkurugenzi wa Chuo hicho Kakongwe Misambano ambaye anashikiliwa na Jeshi la polisi anasema hakufahamu kuhusu wizi wa maji kwenye taasisi yake kwani majengo hayo ameyakodi utetezi ambao unapingwa vikali na maofisa wa DUWASA ambao wanadai kabla ya kubaini uhalifu huo walikutana na upinzani mkali.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mapato cha DUWASA Ester Gilyoma anasema wizi wa maji unaitia hasara mamlaka hiyo na serikali kwani maji yanazalishwa kwa gharama kubwa