Mmoja wa waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Hassan Nassoro Moyo ambaye amekuwa Waziri kwa nyakati tofauti katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pia Waziri wa mambo ya ndani katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefariki dunia leo Alfajiri huko Tanga na anatarajiwa kuzikwa leo majira ya saa kumi nyumbani kwake Fuoni Zanzibar.
Marehemu Hassan pia aliwahi kuwa mjumbe wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi lililoundwa baada ya mapinduzi mwaka 1964 na aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Kazi katika Baraza la kwanza Zaznibar kabla ya muungano.
Mwili wa Mzee Moyo Tayari umewasili Zanzibar leo Asubuhi Agosti 18, 2020 na maziko yatafanyika Saa kumi jioni.