Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango anatarajiwa kuweka jiwe la msingi katika jengo la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini Mtwara leo Julai 26, 2021.
Ujenzi wa Hospitali hiyo unasimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi chini ya Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) ambapo hadi sasa ujenzi huo umefikia 97%, ambapo kukamilika kwa Hospitali hiyo kutapunguza adha kwa wananchi wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kusafiri umbali mrefu kwenda kupata huduma za matibabu ya kibingwa.