Watu wawili waliokua wakisafiri kutoka Kilindi kuelekea Handeni wamejeruhiwa na Nyuki huku mmoja akisadikiwa kupoteza maisha baada ya Nyuki hao kuvamia Magari yaliokwama kutokana na barabara kuharibika kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Kilindi
Wakielezea tukio hilo lililotokea kijiji cha Msente kata ya Jaila wilayani hapa baadhi ya madereva waliotoroka magari yao kwa kuhofia Nyuki hao wamedai kuwa chanzo cha Nyuki hao kuvamia magari na kujeruhi watu ni kutokana na gari moja ya mizigo iliokua imekwama kwenye tope na kusababisha msururu wa Magari hali iliopelekea zaidi ya abiria mia tatu na kushindwa kuendelea na safari.
Hata hivyo baadhi ya abiria walioongea na ITV kwenye stand ya Mabasi yaendayo wilayani Kilindi wakaelezea adha wanayoipata ya barabara hiyo huku nauli zikiongezeka hali inayosababisha wengi kushindwa kusafiri.
Kamera ya ITV iliweza kumtafuta afisa misitu na Nyuki ili kujua mpaka sasa kuna watu wangapi wamejeruhiwa na waliopoteza maisha na mikakati gani wameichukua kunusuru hali hiyo.