Kenya imempoteza mhudumu wa kwanza wa afya kutokana na Covid 19 Dkt Doreen Adisa Lugaliki ambaye ameaga dunia alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Agha Khan jijini Nairobi.
Muungano wa wa madaktari nchini Kenya (KMPDU) umetangaza kuwa Marehemu aliambukizwa virusi vya Corona akiwa kazini alipotangamana na mtu aliyekuwa ameambukizwa COVID 19 katika hospitali ya Nairobi South alikokuwa akihudumu.
Kulingana na Wizara ya Afya marehemu alikuwa na matatizo mengine ya kiafya kabla ya kuambukizwa virusi vya Corona.
Kufikia sasa wahudumu wa kiafya zaidi ya 180 wamethibitishwa kuambukizwa COVID 19 tangu kisa cha kwanza cha Corona kuripotiwa nchini kenya machi 13 mwaka huu.