Back to top

Mwenyekiti wa mtaa Mwanza auawa kwa kuchomwa kisu.

03 June 2020
Share

Mamia wajitokeza kuuaga mwili wa Mwenyekiti wa mtaa wa Nyamanoro mkoani Mwanza Kijungu Magesi aliyefariki baada kuchomwa kisu cha ubavuni na mwanaume mmoja mkazi wa mtaa wake wakati akijaribu kutafuta suluhu baada ya mwanaume huyo kumpiga na kumjeruhi mpenzi wake aliyekimbilia kwa mwenyekiti huyo kuomba msaada.


Tukio hilo limetokea majira ya saa tisa za usiku wakati mwenyekiti huyo alipogongewa mlango na mwanamke mmoja aliyekuwa ameambatana na majirani wengine kwa ajili ya kumtaka kutoa msaada katika tukio la ugomvi baina ya wapenzi wawili .