Mwenyekiti na uongozi wa IPP unasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa mmoja wa waanzilishi wa makampuni ya IPP, Mama Mercy Anna Mengi.
Mama Mercy Anna Mengi amefariki tarehe 31 Oktoba, 2018 katika hospitali ya Mediclinic Morningside, Johannesburg Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu.
Mwili wa marehemu Mama Mercy Anna Mengi unatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam kesho.
Ibada ya kumuaga itafanyika katika kanisa la Azania Front Kesho kutwa, saa 6.00 mchana.
Mazishi yatafanyika Machame Moshi,Kilimanjaro, siku ya jumamosi tarehe 10 Novemba, 2018.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.
AMEN