Back to top

Nguo za ndani za mtumba zakamatwa zikiuzwa sokoni Mbeya.

20 March 2019
Share

Nguo za ndani za mtumba ambazo zimepigwa marufuku nchini, zimekamatwa na maofisa wa Shirika la viwango nchini (TBS) katika soko la Sido jijini Mbeya.

Maofisa wa TBS wamefanya ukaguzi katika soko la SIDO na kukuta nguo hizo zikiuzwa licha ya kupigwa marufuku.

Baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekutwa wakiendelea na biashara hiyo, wamedai kuwa wanaendelea kuuza nguo hizo za ndani za mitumba licha ya kupigwa marufuku na serikali kwa sababu ndizo zinazopendwa zaidi na wateja wao.