#HABARI: Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro amekitaka kikundi cha 'Panya Road' kuacha kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani na kwamba Jeshi hilo limejipanga kukabiliana na watu hao.
.
IGP Sirro amesema hayo wakati alipofanya ziara katika Kata ya Kunduchi Mtongani na Kata ya Kawe jijini Dar es salaam na kuwapa pole watu waliojeruhiwa na kikundi hicho cha 'Panya Road'.