Back to top

Panya Road waibuliwa bungeni, Spika atoa kauli.

15 September 2022
Share

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Tulia Ackson, ameiagiza serikali kuchukua hatua za haraka, kulishughulikia ongezeko la wimbi la matukio ya uhalifu, yanayofanywa na vikundi vya kihalifu maarufu kama 'Panya Road', ambavyo vimekithiri hasa katika mkoa wa Dar es Salaam.


DK Tulia amesisitiza kuwa, serikali inapaswa kulipa uzito zaidi suala hilo, huku akisema kuwa bunge haliwezi kujadili kutokana na kutokukidhi kwa baadhi ya kanuni.


Dk. Tulia amesema hayo, baada ya Mbunge Bahati Ndingo wa Viti Maalum na Mbunge wa Segerea Bona Kamoli kuomba bunge hilo kuhairisha shughuli zake kwa dharura ,kujadili suala hilo.