Rais Dkt. John Magufuli amesema serikali itaendelea kujenga vituo vya afya na kwamba miradi mingi ya afya ilikua ikikwama kutokana na watu wachache kujinufaisha na fedha za miradi hiyo.
Rais Dkt. John Magufuli ameyasema hayo wakati akifungua kituo cha afya cha Madaba kilichopo katika halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 665.