Back to top

Rais Magufuli amteua Dkt. Maduhu Isaac Kazi Mkurugenzi Mtendaji wa TIC

12 July 2020
Share

IKULU CHAMWINO.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Julai, 2020 amemteua Dkt. Maduhu Isaac Kazi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Kazi alikuwa meneja wa idara ya sera za kibajeti na madeni wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Dkt. Kazi anachukua nafasi ya Bw. Godffrey Idelphonce Mwambe.

Uteuzi wa Dkt. Kazi unaanza leo tarehe 12 Julai, 2020.