Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi ametengua uteuzi wa Kamishna Mkuu wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Salum Yussuf Ali ili kupisha uchunguzi wa kina juu ya upotevu wa fedha za makusanyo ya mapato zilizopotea, Dk. Mwinyi ametoa maamuzi hayo alipotembelea ofisi za Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) zilizopo Mazizini Zanzibar ambapo pia alipata fursa ya kuzungumza na uongozi wa Bodi ya Mapato, Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mapato pamoja na uongozi wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA).