Back to top

Serikali kuanzisha vituo vya malezi na makuzi kwa watoto nchi nzima.

24 August 2020
Share

Serikali kupitia Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kuanzisha Vituo vya Malezi na Makuzi ya awali kwa watoto wenye umri kati ya miaka mitatu na minne nchi nzima, ikiwa ni moja ya mikakati ya kumjenga na kumlinda mtoto.
 
Kauli hii imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu alipofanya ziara katika kituo cha malezi na makuzi ya awali ya mtoto cha Nyerere kilichoko Igombe Ilemela jijini Mwanza.

Dkt. Jingu amesema Vituo vya malezi na makuzi kwa watoto ni muhimu sana ili kuhakikisha wanapata huduma bora zitakazowezesha uchechemuzi wa bongo zao kuwekwa katika mazingira mazuri ya ukuaji.

 “Vituo vya malezi na makuzi ya awali kwa watoto vinalenga kutoa fursa kwa wazazi na walezi kutekeleza shughuli za kiuchumi” alisema


Naye Afisa Mradi Kituo cha Malezi na Makuzi cha Nyerere Julieth Joseph amesema kuwa Kituo cha Malezi na Makuzi ya Mtoto cha Nyerere kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2016 mpaka mwaka 2019 kimefanikiwa kuwaandaa watoto zaidi ya 400 kabla ya kuwapeleka katika Shule za awali.