Serikali inatarajia kufungua Mahakama kuu Kigoma itakayowasaidia wananchi kuondokana na usumbufu wa kulazimika kusafiri kwa ajili ya kukata rufaa wakitafuta haki,katika Mahakama kuu Kanda ya Tabora ambako wengi hushindwa kwenda na hivyo kupoteza haki.
Kaimu Hakimu mkazi Mfawidhi mkoa wa Kigoma flora Mtarania amesema serikali inatarajia kufungua mahakama hiyo ambayo itakuwa mkombozi kwa wananchi wa mkoa wa Kigoma ambao wengi wao ni maskini ambao wamekuwa wakikosa uwezo wa kusafiri hadi mkoani Tabora.
Akizindua bodi mpya ya Parole mkuu wa mkoa wa Kigoma Bgigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga ameiagiza bodi hiyo kuhakikisha inatoa elimu kwa wananchi kuhusu kazi za bodi ikiwa ni pamoja na masuala ya kisheria ili kusaidia kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani.