Shule kongwe ya msingi Bugarama iliyoko katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama yenye wanafunzi zaidi ya 2,300 inakabiliwa na msongamano wa wanafunzi madarasani unaosababishwa na upungufu wa madarasa.
Kufuatia hali hiyo wadau wa elimu wilayani Kahama wametoa mifuko ya saruji 112 kwa lengo la kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa katika shule hiyo.
.
Nao baadhi ya wazazi wenye watoto wanaosoma katika shule hiyo wameshukuru kwa msaada huo ambao umewapunguzia michango huku Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela akiahidi kumalizwa kwa tatizo hilo.