Back to top

TANESCO KUZALISHA UMEME KWA VYANZO MSETO VYA NISHATI

16 September 2022
Share

Shirika la umeme Tanzania Tanesco limesema limeanza mikakati ya kuweka mazingira bora ya kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo mseto vya Nishati, ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, ambayo yamesababisha uwepo wa upungufu wa maji katika baadhi ya vyanzo vya uzalishaji wa umeme.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wateja Tanzania Tanesco, Bw.Martin Mwambene amesema mpaka sasa kituo cha Ubungo chenye uwezo wa Megawati 112 kinacho zalisha umeme wa gesi kimekamilika na mradi wa Kinyerezi 1 Extension ambao utaingiza jumla ya Megawati 185 katika Gridi ya Taifa unatazamiwa kukamilika na kuongeza nguvu za uzalishaji.
 
Mwambene ameongeza kuwa Tanesco inaendelea na mikakati ya kuhakikisha inaongeza vyanzo vingine vya uzalishaji umeme kwa kutumia vyanzo vya Nishati Jadidifu vitakavyoweza kuchangia na kufikia Megawati 2000