Back to top

TANZANIA MWENYEJI KONGAMANO LA 'APIMONDIA' 2027

04 September 2024
Share

Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la Wafugaji Nyuki Duniani (Apimondia) litakalofanyika mwaka 2027. 

Hayo yamebainika Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Dunstun Kitandula, katika kipindi cha maswali na majibu na  ameongeza kuwa serikali imejipanga kwa njia mbalimbali kuhakikisha Watanzania wanashiriki kikamilifu, pamoja na kunufaika na Kongamano hilo ikiwa ni pamoja na kuunda Kamati ya Maandalizi ya Kitaifa ambayo inajumuisha wajumbe kutoka serikalini na sekta binafsi.


Aidha ameainisha mikakati mingine ya serikali, ni kujumuisha uhamasishaji wa wananchi katika ufugaji, uzingatiaji ubora na kufungua masoko mapya ya mazao ya nyuki duniani.