Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA), imesema kuanzia Januari 01, 2023, itachukua usimamizi wa eneo ambalo lilikuwa likisimamiwa na Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena (TICTS) katika bandari ya Dar es Salaam huku ibainisha kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya mkataba wa TICTS kuisha muda wake.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi wa TPA, Juma Kijavara, katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika Bagamoyo mkoani Pwani na kusisitiza kuwa huduma zitakuwa bora zaidi ya awali na ajira za wafanyakazi wa TICTS zitakuwa salama.