Back to top

TRRH YATUMIA HAJA KUBWA KUGUNDUA KIFUA KIKUU.

24 October 2023
Share

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke(TRRH) imeanza kutoa huduma za kiuchunguzi kwa wahisiwa  wa kifua kikuu kupitia kipimo cha haja kubwa kwa makundi maalumu ambayo ni watoto chini ya miaka 5 ambao hawana uwezo wa kutoa sampuli ya makohozi ,wagonjwa wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi, na Wagonjwa waliolala kitandani muda mrefu waliozidiwa.

Dr. Rose Chagama, mtaalamu wa kifua kikuu na Ukoma kutoka hospitali hiyo, amesema kuwa kipimo hicho ni kipya kwa Tanzania na kwa Temeke hospitali huduma imeanza kutolewa mwezi wa tisa mwishoni kuelekea mwezi wa kumi mwaka huu.

Dr. Chagama amesema kuwa, hichi kipimo cha Kifua kikuu kupitia haja kubwa ni kipimo mahususi kwa makundi maalumu.kipimo hiki kinatumia Vinasaba  na kimefanikiwa kugundua wagonjwa kadhaa ikiwemo mtoto wa miezi 5.