Back to top

Tumieni Shirika la Posta Tanzania kusafirisha bidhaa-Dkt.Chaula.

04 June 2020
Share

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainab Chaula amezikumbusha taasisi za Serikali kutumia huduma za Shirika la Posta Tanzania (TPC) kusafirisha bidhaa, vifurushi na vipeto kwa usalama zaidi.

Dkt. Chaula ameyasema hayo wakati wa kikao cha Menejimenti ya Wizara yake na viongozi wa TPC wakiongozwa na Posta Masta Mkuu wa TPC, Hassan Mwang’ombe kilichofanyika kwenye ukumbi wa Wizara hiyo uliopo Mtumba, Mji wa Serikali,Dodoma.

Dkt. Chaula alisema kuwa TPC imepewa dhamana kisheria kuwa msafirishaji mkuu wa barua, vifurushi, vipeto na bidhaa mbali mbali kwa mujibu wa sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Na. 19 ya mwaka 1993 iliyoanzisha Shirika hilo nani Shirika la umma ambapo Serikali imewekeza.