Back to top

TUTAHAKIKISHA RASILIMALI YA WANYAMAPORI INADUMU – CHANA

16 October 2024
Share

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amefanya ziara katika makao makuu ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Njiro - Arusha, ambapo amebainisha umuhimu wa Tafiti za Wanyamapori  katika kupata  takwimu za Kisayansi zinazotumika kufanya maamuzi.

Akizungumza katika kikao na Menejimenti ya TAWIRI Mhe. Chana amesema Serikali inatumia takwimu za kisayansi kufanya maamuzi yaliyojikita kuimarisha uhifadhi wa Wanyamapori ili kuwa na utalii endelevu.

"Tunahakikisha rasilimali hii ya Wanyamapori ipo kwa kizazi cha leo na kijacho ambapo  matumizi ya takwimu za kisayansi ni dira katika uhifadhi  amesisitiza Waziri Chana.

Mkurugenzi Mkuu TAWIRI Dkt.Eblate Mjingo amesema takwimu za tafiti zinasaidia kunadi Utalii ikiwa ni pamoja na kuelekeza  namna bora ya kufanya Utalii sambamba na kuimarisha uhifadhi.

Aidha, Pamoja na mambo mengine Waziri Chana amepokea taarifa mbalimbali za utendaji kazi wa Taasisi hiyo.

Kikao hicho kimehudhuriwa  na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Utalii, Nkoba Mabula, Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Dkt.  Thereza Mugobi, wawakilishi kutoka Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii na Maafisa Waandamizi kutoka TAWIRI.