Back to top

TUZO YA MWALIMU BORA MILAMBO SEC. YAZINDULIWA

12 October 2024
Share

Umoja wa wanafunzi waliosoma shule ya sekondari Milambo, iliyoko mkoani Tabora wamezindua  zawadi ya Mwalimu bora wa Mwaka  kwa shule hiyo.

Uzinduzi huo umefanyika kijijini Mwitongo, Butiama mkoani Mara alikozaliwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa umoja huo, Bw. Abdul-Razak Badru,  mshindi atakua akipewa zawadi na fedha taslimu.
Aidha, zawadi ya kwanza ya mwalimu bora  kwa heshima  imeenda kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambae aliwahi kufundisha shule hiyo ya Milambo wakati huo ikiiitwa St Merrys.

Zawadi hiyo imepokelewa na mtoto wa Mwalimu Nyerere, Bw. Madaraka Nyerere kwaniaba ya familia.