Halmashauri ya Mpimbwe, wilaya ya Mlele mkoani Katavi inakabiliwa na uhaba mkubwa wa vifaa vya kupimia joto la mwili kwa abiria wanaotoka nje ili kubaini kama mhusika ana maambukizi ya virusi vya Corona au la.
Mganga Mkuu wa halmashauri hiyo Dakta Omar Sukari amesema kutokana na ukosefu huo abiria hao wanalazimika kutumia vitakasa mikono tu, hali inayodhoofisha mapambano dhidi homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.
Amesema halmashauri ina vipima joto vitano tu kati ya kumi na sita vinavyohitajika hali inayowalazimu wataalamu wa afya kutumia njia mbadala kutambua wagonjwa, ambayo hata hivyo hakuieleza.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bwana Juma Homera aliyekuwa akikagua utekelezaji wa maagizo yanayolenga kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona katika halmashauri hiyo amemtaka Mganga Mkuu huyo afanye kila jitihada ili vifaa hivyo vipatikane.