Back to top

UJENZI UWANJA MPYA WA NDEGE HIFADHI YA NYERERE KUONGEZA WATALII

30 October 2023
Share

Ujenzi wa Uwanja cha ndege wa Mtemere katika Hifadhi ya Taifa Nyerere wenye urefu wa Kilometa 1.8, unaotekelezwa na Mradi Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) unatarajiwa kuwa chachu katika kuongeza idadi ya Watalii pamoja na kuongeza pato la Taifa kupitia sekta ya Utalii nchini.

Hayo yamebainishwa na Mwakilishi wa Mradi wa REGROW katika Hifadhi ya Taifa Nyerere, Afisa Mhifadhi Daniel Mathayo ambapo amesema uwanja uliopo sasa una uwezo wa kupokea ndege 12 ambapo kukamilika kwa Ujenzi wa Uwanja mpya utakaokuwa na uwezo wa kupokea kwa wingi ndege kubwa ambazo zitakuwa na uwezo wa kubeba abiria Zaidi ya 100 hatua itakayochochea ongezeko la mapato katika hifadhi hiyo.

Kwa upande wake Mhandisi Mshauri wa uwanja wa ndege wa Mtemere Edson Shayo kutoka Kampuni ya Howard amesema kuwa Mradi huo ulioanza Juni 12, 2023 unatarajiwa kukamilika Agosti 2024 na mpaka sasa mpaka umefikia asilimia 21.7.

Mmoja wa Rubani wa ndege zinazosafirisha Watalii Hifadhi ya Taifa Nyerere,  Bw.Khalid Amarjit ameipongeza REGROW kwa kutekeleza ujenzi huo ambapo amesema kuwa kukamilika kwa uwanja mpya wa ndege kutawarahisishia wao kutopata changamoto kwa kuwa uwanja uliopo kwasasa ni mdogo.