Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imewataka wanahabari kutumia kalamu zao vizuri kuelimisha na kuhabarisha umma kuhusu athari za dawa za kulevya, lakini kama wanajamii wana wajibu wa kutoa taarifa kwa mamlaka pale kunapotokea uhalifu au matatizo kuhusu masuala ya Dawa za Kulevya.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya) Bi.Florence Khambi katika kikao cha mpango kazi na waandishi wa habari Morogoro.
Bi.Florence Khambi amesema sheria imemtambua mtumiaji wa dawa za kulevya kama mgonjwa lakini itategemea na kiwango cha dawa alizokutwa nazo ambazo pia zitaamua kama yeye ni mtumiaji au ni mfanyabiashara.
Aidha Bi.Florence ameongeza kuwa mbali na shisha kuonekana sio dawa za kulevya inayotambulika kisheria bado baadhi ya watu wamekuwa wakitumia njia hiyo kuongeza watumiaji wa Dawa za Kulevya.