Back to top

URUSI : MAUAJI YA KIRILLOV NI 'TENDO LA KIGAIDI'

17 December 2024
Share

Luteni Jenerali wa ngazi ya juu Igor Kirillov, ambaye ni Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi cha Nyuklia, Biolojia, Kemikali (NBC), katika Jeshi la Urusi na Msaidizi wake wameuawa katika mlipuko uliotokea mjini Moscow.

Jenerali huyo alikuwa akiondoka kwenye makazi mapema Jumanne wakati kifaa kilichofichwa kwenye skuta (Scooter) kilipolipuka, Kamati ya uchunguzi ya Urusi imeeleza kuwa kuuawa kwa Luteni Jenerali Kirillov kuwa ni "kitendo cha kigaidi".

Siku ya Jumatatu, huduma ya usalama ya Ukraine ilimshtaki Kirillov bila kuwepo mahakamani, ikisema kwenye Telegram kwamba "alihusika na matumizi makubwa ya silaha za kemikali zilizopigwa marufuku". 

Serikali ya Ukraine bado haijatoa maoni yoyote kuhusu kifo cha jenerali huyo.