Back to top

Wachimbaji wa chumvi Uvinza waomba serikali kuanzisha masoko.

31 July 2019
Share

Wachimbaji wadogo wa madini ya chumvi pamoja na wananchi katika kijiji cha Uvinza wilayani Uvinza mkoani Kigoma wameiomba serikali kukaa upya na mwekezaji aliyewekeza katika mgodi huo ili kuangalia upya namna bora ya kuanzishwa kwa masoko makubwa ya chumvi katika maeneo yao tofauti na ilivyo sasa hali inayosababisha wananchi wa wilaya ya Uvinza kukosa fursa za kiuchumi na kunufaika na madini hayo.

Wakizungumza mbele ya waziri wa Madini Mheshimiwa Dotto Biteko wamesema masoko makubwa yalianzishwa nje ya wilaya ya Uvinza yamesababisha wananchi pamoja na wachimbaji wadogo wa chumvi kushindwa kunufaika na uwepo wa machimbo hayo jambo linalosababisha kuendelea kudumaza uchumi wa maeneo yao.

Akijibu maombi ya wananchi hao,waziri wa madini mheshimiwa Dotto Biteko ameagiza wilaya ya Uvinza pamoja na menejimenti ya kiwanda cha chumvi cha Uvinza kuanzisha soko la madini ya chumvi ili kuwasaidia wananchi kunufaika na uwepo wa madini hayo kama maeneo mengine