Mkoa wa Mtwara umetajwa kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa hali inayotokana na baadhi ya wanawake walioshika ujauzito kugoma kunywa dawa za kuongeza damu na zile za folic acid kwa madai ya kuogopa kuzaa watoto wakubwa na hivyo kusababisha kuzaa watoto wenye matatizo ya kiafya ikiwemo vichwa vikubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mganga Mkuu wa mkoa wa Mtwara Cilivia Mamkwe amekiri kuwapo kwa changamoto hiyo ambayo inatokana na uelewa mdogo katika jamii.